Friday, August 24, 2018

ZIARA YA KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WORLD METEOROLOGICAL ORGANISATION – WMO) PROF. PETTERI TAALAS KATIKA OFISI ZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA TAREHE 22 AGOSTI, 2018


Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa yanayohusiana na ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na namna mifumo hii inavyoathiri mazingira yetu. Shirika hufanya kazi zake kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama (National Meteorolgical and Hydrological Services - NMHSs) ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni mwakilishi rasmi wa shirika hili hapa nchini.
Katibu Mkuu wa WMO amefanya ziara katika ofisi za TMA ili kujionea shughuli za hali ya hewa na namna ambavyo WMO inaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali yahusuyo hali ya hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa vya hali ya hewa. Aidha aliipongeza TMA katika juhudi zake  za utekelezaji  wa programu za WMO na kuzisaidia nchi zingine za Afrika. Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni taasisi ya mfano Afrika katika utoaji wa huduma bora za hali ya hewa
Nae mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi  aliwashukuru Prof. Taalas kwa uamuzi wake wakutembelea Tanzania na alimuahidi kuwa Tanzania kupitia TMA itaendelea kutekeleza makubaliano yote ya kimataifa yahusuo huduma za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa program za WMO
Ikumbukwe kuwa WMO huratibu na kusaidia katika kuboresha huduma za hali ya hewa katika nchi kama vile kuanzisha mitandao ya ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuweka miongozo inayosaidia utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa viwango na ubora wa kimataifa n.k
Kupitia WMO Tanzania na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imenufaika na kuongezewa uwezo kupitia mafunzo, miundombinu ya hali ya hewa, hushiriki kikamilifu katika shughuli za jopo la sayansi la kimataifa la ufuatiliaji wa mabadiliko ya hali ya hewa (Intergovernmental Pannel on Climate Change - IPCC). Pia, kushiriki katika shughuli za kongamano la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi hasa masuala ya kisera (United Nations Framework for Climate Change Conference - UNFCCC) ambapo mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea Tanzania hujumuishwa katika makubaliano ya kimataifa kwa ajili ya utekelezaji kimataifa na kitaifa kwa faida ya nchi yetu.

Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akisaini kitabu cha wageni, kukutana na wenyeji wake sambamba na  picha ya pamoja na menejimenti ya TMA 

   Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA Bw. Chuki Sangalugembe kuhusiana na mtambo mkubwa wa kompyuta (Computer Cluster) namna unavyosaidia katika uandaaji wa taarifa za hali ya hewa. 

Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akichangia jambo baada ya kupata maelezo ya mfumo wa kisasa utoaji taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wakati alipotemebelea ofisi za hali ya hewa zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere. hewa.

    

  Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akishuhudia na kushiriki mkutano wa kuandaa utabiri wa siku unaofuatilia hali mbaya ya hewa kwa nchi za Afrika mashariki zilizoko katika Bonde la Ziwa Victoria. 
  Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa meneja wa kituo kikuu cha utabiri Bw. Samuel Mbuya namna ya kuandaa utabiri wa hali ya hewa 
  Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo kutoka kwa meneja wa mtandao wa vituo vya hali ya hewa nchini Bi. Hellen Msemo (hayupo pichani) kuhusiana na studio ya TMA inayohusika katika kurekodi utabiri wa hali ya hewa wa kila siku. 
   Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo ya namna ya kuwaandikisha wakulima katika mfumo wa utoajia taarifa za hali ya hewa kilimo kupitia simu za mkononi uitwao FARMSMS kutoka kwa meneja wa huduma za matumizi ya taarifa za hali ya hewa Bw, Isack Yonah 
    Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo ya namna ya uhifadhi wa takwimu za muda mrefu za hali ya hewa kwa njia ya kidigitali(kisasa) kupitia mfumo wa CLIDATA kutoka kwa mtaalamu wa kuhifadhi takwimu za hali ya hewa



No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...