Tuesday, August 28, 2018

WANASAYANSI WA HALI YA HEWA NCHINI (METEOROLOGISTS) WAKUTANA KUANDAA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA MWEZI OKTOBA HADI DESEMBA 2018

WANASAYANSI WA HALI YA HEWA NCHINI (METEOROLOGISTS) WAKUTANA KUANDAA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA MWEZI OKTOBA HADI DESEMBA 2018

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA)  ikiwa katika maandalizi ya kutoa utabiri/mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli imeandaa mkutano wa wanasayansi wa hali ya hewa (meteorologists) kujadili rasimu ya mwelekeo huo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amewataka wataalam hao kuandaa kwa pamoja na kupitia mfumo mzima wa uaandaaji ili kujiridhisha  na utabiri utakao tolewa hapo baadae sambamba na kutoa mapendekezo ya uboreshaji katika maandalizi mengine ya misimu ijayo. Aidha Dk. Kijazi aliwapongeza wanasayansi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa utabiri wenye viwango vya juu vya usahihi kwa zaidi ya asilimia 80 na kuwataka waendelea kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kufikia juu ya asilimia 90.

Hii ni mara ya kwanza kwa TMA kuwakutanisha wanasayansi kutoka vituo vyote nchini ambapo awali kazi ya uandaaji utabiri ilikuwa ikifanywa na wanasayansi wa makao makuu na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) pekee

TMA inatarajia kutoa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa mikoa inayopata mvua mara mbili kwa mwaka tarehe 06 Septemba 2018.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...