Friday, March 24, 2017

NAIBU WAZIRI AZUNGUMZIA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI KWA WANAHABARI

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akiongea na  vyombo vya habari (hawapo pichani)
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu swali kwa  vyombo vya habari (hawapo pichani)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Agnes Kijazi akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
Baadhi ya wanahabari katika pichaMAADHIMISHO YA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI

TAREHE 23 MACHI, 2017

Kila mwaka ifikapo tarehe 23 Machi nchi wanachama 190 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani hujiunga kuadhimisha kuzaliwa kwa Shirika hilo lililoanzishwa tarehe 23 Machi, 1950 kulingana na kauli mbiu teule. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ’Tuyaelewe mawingu na umuhimu wake’- ”(Understanding clouds)”.
Katika kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani (WMD), Shirika la Hali ya Hewa Duniani  limetambua umuhimu wa kuongeza uelewa wa mawingu ili kujua zaidi mchango wake katika mzunguko wa maji kati ya nchi kavu, baharini na angan,i na uhusiano wake na hali ya hewa ya muda mfupi na mrefu. Kama inavyojulikana kuwa mawingu yana umuhimu mkubwa sana katika mifumo ya hali ya hewa ya dunia na hivyo elimu juu ya tabia ya mawingu itasaidia katika kutabiri hali ya hewa na kutambua mabadiliko ya tabia nchi kwa wakati ujao. Wahenga huwa wanasema, Dalili ya Mvua ni Mawingu.
 
Kama ilivyo kwa wanachama wengine, Tanzania inaungana nao kuadhimisha siku hii inayofikia kilele leo tarehe 23 Machi, 2017 kwa kuwakaribisha wananchi wote kutembelea vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona shughuli zitolewazo na Mamlaka na kujifunza. Aidha, Mamlaka itambelea na kutoa elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbali mbali nchini kupitia ofisi zake zilizopo nchi nzima. Kutoa makala  za siku hiyo kwenye magazeti, vipindi kwenye radio, televisheni na mitandao ya kijamii kuhusu elimu juu ya mawingu na sayansi hali ya hewa kwa ujumla, hii itasaidia kuongeza wigo wa elimu kwa umma hususani mashuleni.

Tunawatakia maadhimisho mema ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani

’Tuyaelewe mawingu na umuhimu wake’
(Understanding Clouds)

Kupata makala za Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa  na Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi ingia humu  http://www.meteo.go.tz/news/74


No comments:

Post a Comment