Sunday, October 22, 2017

MHE. JENISTA MHAGAMA(MB) AKUTANA NA UONGOZI WA TMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) katika picha ya pamoja na uongozi wa TMA, kushoto kwake ni mwenyeji wake Dkt. Agnes Kijazi na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig, Jen. Mbazi Msuya, Mratibu wa Mradi Bw. Alfei Daniel, Mkurugenzi wa ofisi ya Hali ya Hewa Zanzibar Bw. Mohamedi Ngwali (pembeni ya Dkt.Kijazi)


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi akitoa maelezo kwa Mh. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Ulemavu) Jenista Mhagama (MB) jinsi Mradi huo ulivyochagia katika Uboreshaji wa upatikanaji wa takwimu na usahihi wa taarifa za hali ya hewa ikiwemo Tahadhari za Awali.Waziri wa Ofisi ya waziri Mkuu:Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) atembelea TMA kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Mfumo wa Tahadhari za Majanga yanayosababishwa na Mabadiliko ya Hali ya Hewa unaofadhiliwa na UNDP. Katika Utekekelezaji wa Mradi huo TMA imejengewa uwezo katika nyanja za wataalamu na miundombinu ya hali ya hewa. Vituo 36 vya hali ya hewa vinavyojiendesha vyenyewe vimefungwa katika maeneo mbalimbali nchini. Uboreshaji huu wa huduma unalenga kuongeza ufanisi katika sekta mbalimbali za kiuchumi kwa ustawi wa jamii.