Friday, August 12, 2016

WADAU MBALIMBALI WAKUTANA KUJADILI UMUHIMU WA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA SEKTA YA AFYA





 Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania TMA, wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto na Taasis ya kusimamia Anga na Bahari kutoka Marekani (NOAA) wameandaa warsha ya siku tatu kuanzia tarehe 10 mpaka 12 Agosti 2016 yenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya hali ya hewa na  sekta ya afya ili kujadili changamoto zitokanazo na hali ya hewa zinazokabili sekkta ya afya.
Akifungua warsha hiyo katika ukumbi wa Ramada kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA ambaye pia ni mjumbe wa Bodi Prof. Msola alizungumzia umuhimu wa kukaa na wadau husika ili kuweza kusikia mahitaji yao kwa maendeleo ya nchi na ulimwenguni kwa ujumla, ikizingatiwa kwamba ulimwenguni kote kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa hivyo ni muhimu kutambua maeneo mahususi ya kutiliwa mkazo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka TMA Dkt. Ladislaus Changa alishukuru kwa niaba ya TMA na Serikali ya Tanzania kwa  kupata hiyo nafasi ya kukutana na wadau kupitia ufadhili wa NOAA na kuahidi ushirikiano mkubwa kati ya TMA na Wizara ya afya,Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto sambamba na taasisi zingine zinazoshughulikia masuala ya afya, ushirikiano huo utasaidia uboreshaji wa huduma zitolewazo za hali ya hewa kwa sekta ya afya.
Mwakilishi kutoka NOAA Dkt.Wassila Thaw alielezea umuhimu wa wao kufadhili na kushiriki ni pamoja na kuhakikisha maazimio yote ya warsha hii yanatafutia ufumbuzi kwa vile moja ya majukumu ya NOAA ni pamoja na kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinatumika katika sekta za afya kwa matokea chanya.
Warsha hii imejumuisha wadau kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya Kilimo na Mifugo, IRI,ICPAC Kenya,NOAA, IRI, NASA, Chuo Kikuu Chicago kutoka Marekani, Taasisi ya Hali ya Hewa Ethiopia, Madagascar,Kenya, Uganda,Mozambique, Wizara za Afya Kenya, Ethiopia, Uganda, WMO, WHO  pamoja na Chuo Kikuu Muhimbili.

IMETOLEWA NA MONICA MUTONI, AFISA UHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...