Wednesday, August 31, 2016

CHUO CHA HALI YA HEWA KIGOMA CHA SHEREHEKEA MAHAFALI YA NNE YA KOZI YA 'AERONAUTICAL METEOROLOGY' YALIYOFANYIKA UBUNGO PLAZA, TMA TAREHE 26 AGOSTI 2016

Mgeni rasmi na Mkurugenzi Mkuu TMA akigawa cheti kwa mmoja wa wahitimu
Mgeni rasmi na Mkurugenzi Mkuu TMA akigawa cheti na zawadi kwa mhitimu aliyefanya vizuri zaidi katika kozi hiyo
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma Bw. Peter Mlonganile akitoa hotuba yake katika mahafali
Kiongozi wa wahitimu akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya wahitimu wengine

NATIONAL METEOROLOGICAL AGENCY OF ETHIOPIA DELEGATION VISIT AT TMA


Monday, August 22, 2016

KUPATWA KWA JUA TAREHE 01 SEPTEMBA, 2016

                                                               Picha: Mfano wa kupatwa kwa jua

Hali ya kupatwa kwa jua ni tukio la aina yake linatokea pale ambapo miali ya jua hupungua hadi kutoonekana tena na kusababisha sehemu ya uso wa dunia kuwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu katika eneo husika.

Kupatwa kwa jua kunatokea wakati dunia, mwezi na jua vinapokaa kwenye mstari mmoja mnyoofu wakati mwezi unakuwa kati ya dunia na jua. Hali hiyo inapotokea kunajengeka kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia. Kivuli hicho hufunika sehemu  tu ya  uso wa dunia. Kutokana na hali hiyo kupatwa kwa jua kwa maeneo yaliyo mengi kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.

2.Maelezo ya Kisayansi

Wanasayansi wanaelezea kupatwa kwa jua kama tukio linalotokea na kuonekana katika namna tofauti tofauti mfano; ni kupatwa kwa jua kikamilifu hali ambayo hutokea pale miali ya jua inapotea kabisa katika eneo husika kwa kipindi kifupi. Hali hii inapotokea eneo husika linakosa kabisa mwanga wa jua na kuwa giza.

Aina ya pili  ni kupatwa kwa jua kisehemu;  hii hutokea wakati eneo kubwa linapopata upungufu wa mwanga wa jua hali ambayo hupungua kadiri mtu anavyokuwa mbali na kitovu cha mstari wa kupatwa kwa jua. Kiwango cha upungufu wa mwanga wa jua hutegemea umbali mtu alipo kutoka kwenye kitovu cha kivuli kamili.

Aina nyingine ni kupatwa kwa jua kipete; hali hii inapotokea mwezi huzuia mwanga wa jua kufika kwenye dunia kwa vile huweka duara la kivuli cha mwezi kwenye dunia na hivyo mwanga wa  jua huonekana kama pete. Inatarajiwa kuwa aina hii ya kupatwa kwa jua ndiyo itakayojitokeza  tarehe 1 Septemba 2016 katika baadhi ya maeneo ya Bara la Afrika. Kwa hapa nchini hali hiyo inatarajiwa kujitokeza katika sehemu kubwa ya maeneo ya mikoa ya Nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya kusini mwa nchi.  Hata hivyo,  watu katika maeneo mengine ya nchi yaliyokaribu na ukanda huo wanatarajiwa kuona kupatwa kwa jua kisehemu yaani upungufu wa mwanga wa jua kwa dakika kadhaa, imetabiriwa takriban kakika tatu (3).  Jua linatarajiwa kupatwa wakati wa asubuhi kati ya saa tatu asubuhi na saa sita.

3. Athari zake kwa Hali ya Hewa.

Kwa ujumla hakuna athari zozote kubwa zinazotarajiwa kutokana na hali hiyo.  Hata hivyo, upo uwezekano wa kupungua kwa viwango vya joto katika maeneo ambapo kupatwa kwa jua Kipete kutajitokeza.  Kwa kuwa tukio hilo la kupatwa kwa jua huchukua muda wa dakika chache tu hali ya joto itapungua kwa haraka katika kipindi kifupi na baadae kuongezeka kurudi katika hali yake ya kawaida. Viwango vya kupungua kwa joto vitatofautiana kulingana na umbali kutoka eneo la kupatwa kwa jua

4. Upekee wa tukio la kupatwa kwa jua

Tukio hili hutokea au kujirudia mara chache sana katika eneo husika. Inakadiriwa kuwa inaweza kuchukua kati ya miaka 350 hadi 400 kwa hali hiyo kujitokeza tena katika eneo litakapotokea mwaka huu 2016. Hii ndio sababu kwa watu wa eneo husika na wanasayansi  hili ni tukio la muhimu na kumbukumbu muhimu ya maisha.

Mamlaka ya hali ya hewa inaendelea kufuatilia na itatoa taarifa za mabadiliko yoyote yanayoweza kujitokeza katika hali ya hewa kulingana na tukio hili la kupatwa kwa jua.Dk. Agnes L. Kijazi
MKURUGENZI MKUU

Wednesday, August 17, 2016

Friday, August 12, 2016

CLIMATE AND HEALTH WORKSHOP, RAMADA HOTEL RESORT,10 TO12 AUGUST 2016

Participants of Climate and Health Workshop in a group photo aligned with he guest of honor Prof Suzan Nchimi Msola during an opening ceremony which took place on 10th August 2016 in Dar es Salaam.
Representative from NOAA Dr. Wasilla Thaiw adressing the audience during an opening ceremony which took place on 10th August 2016 in Dar es Salaam.
Workshop participants during an opening ceremony which took place on 10th August 2016 in Dar es Salaam.
Add caption
Dr. Ladisalus Chang'a TMA Director of Researh and Applied adressing the audience on behalf of TMA Director General during an opening ceremony which took place on 10th August 2016 in Dar es Salaam.
Workshop participants
Prof Suzane Msola guest of honor and TMA board member adressing the audience on behalf of chairperson of Ministrial Advisory Board during an opening ceremony which took place on 10th August 2016 in Dar es Salaam.

WADAU MBALIMBALI WAKUTANA KUJADILI UMUHIMU WA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA SEKTA YA AFYA

 Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania TMA, wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto na Taasis ya kusimamia Anga na Bahari kutoka Marekani (NOAA) wameandaa warsha ya siku tatu kuanzia tarehe 10 mpaka 12 Agosti 2016 yenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya hali ya hewa na  sekta ya afya ili kujadili changamoto zitokanazo na hali ya hewa zinazokabili sekkta ya afya.
Akifungua warsha hiyo katika ukumbi wa Ramada kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA ambaye pia ni mjumbe wa Bodi Prof. Msola alizungumzia umuhimu wa kukaa na wadau husika ili kuweza kusikia mahitaji yao kwa maendeleo ya nchi na ulimwenguni kwa ujumla, ikizingatiwa kwamba ulimwenguni kote kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa hivyo ni muhimu kutambua maeneo mahususi ya kutiliwa mkazo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka TMA Dkt. Ladislaus Changa alishukuru kwa niaba ya TMA na Serikali ya Tanzania kwa  kupata hiyo nafasi ya kukutana na wadau kupitia ufadhili wa NOAA na kuahidi ushirikiano mkubwa kati ya TMA na Wizara ya afya,Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto sambamba na taasisi zingine zinazoshughulikia masuala ya afya, ushirikiano huo utasaidia uboreshaji wa huduma zitolewazo za hali ya hewa kwa sekta ya afya.
Mwakilishi kutoka NOAA Dkt.Wassila Thaw alielezea umuhimu wa wao kufadhili na kushiriki ni pamoja na kuhakikisha maazimio yote ya warsha hii yanatafutia ufumbuzi kwa vile moja ya majukumu ya NOAA ni pamoja na kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinatumika katika sekta za afya kwa matokea chanya.
Warsha hii imejumuisha wadau kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya Kilimo na Mifugo, IRI,ICPAC Kenya,NOAA, IRI, NASA, Chuo Kikuu Chicago kutoka Marekani, Taasisi ya Hali ya Hewa Ethiopia, Madagascar,Kenya, Uganda,Mozambique, Wizara za Afya Kenya, Ethiopia, Uganda, WMO, WHO  pamoja na Chuo Kikuu Muhimbili.

IMETOLEWA NA MONICA MUTONI, AFISA UHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.