Tuesday, June 21, 2016

TAARIFA KWA UMMA

YAH: KUSIKILIZA KERO NA KUPOKEA MAONI MBALIMBALI YA WANANCHI KUHUSU HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imeandaa siku ya Alhamis, saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana, Tarehe 23 Juni 2016 ili kusikiliza kero sambamba na kupokea maoni mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini. Kazi hii  itafanyika katika ukumbi wa Mikutano, ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza-Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kazi hii ni utekelezaji wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini kwa mwaka 2016. 
‘Wananchi wote mnakaribishwa’
IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO- MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment