Wednesday, June 29, 2016

BODI YA USHAURI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YAFANYA ZIARA YA KUANGALIA UFANISI WA KAZI ZA TMA-DAR ES SALAAM

Picha (hapo juu) ni wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TMA kwenye ziara ya kuangalia utendaji kazi wa Mamlaka katika kituo cha radar ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu-Dar es Salaam, tarehe 27 Juni 2016. Ziara hiyo iliongozwa na mwenyekiti wa Bodi Dkt. Buruhani Nyenzi.
Picha (hapo juu) ni wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TMA kwenye ziara ya kuangalia utendaji kazi wa Mamlaka katika ofisi ya hali ya hewa iliyopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa (JNIA), Dar es Salaam, tarehe 27 Juni 2016. Ziara hiyo iliongozwa na mwenyekiti wa Bodi Dkt. Buruhani Nyenzi.
 Picha (hapo juu) ni wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TMA kwenye ziara ya kuangalia utendaji kazi wa Mamlaka katika ofisi mbalimbali zilizopo makao makuu, Dar es Salaam, tarehe 27 Juni 2016. Ziara hiyo iliongozwa na mwenyekiti wa Bodi Dkt. Buruhani Nyenzi.



Wednesday, June 22, 2016

WORKSHOP ON TSUNAMI AWARENESS AND PREPAREDNESS AND STANDARD OPERATING PROCEDURES FOR TSUNAMI WARNING AND EMERGENCY RESPONSE IN TANZANIA AT THE PRE-IOWAVE16 TRAINING HELD AT PROTEA COURTYARD HOTEL IN DAR ON 20TH TO 24TH JUNEE 2016

Permanent Secretary, Ministry of Works, Transport and Communications (Transport sector), Eng. Leonard M. Chamuhiro adressing  his speech during a workshop.
Acting Director General -TMA Dr. Ladislaus Chang'a  adressing  his thanks remarks during a workshop.
Mr. Ardito Kodijat, representative of IOC/UNESCO- Indian Ocean Tsunami Information Centre
The main objective of the workshop was to enhance the understanding of Tsunami hazard, tsunami risk as well as Standard Operating Procedures (SOPs) for tsunami warning and emergency response from national to community level.

Tuesday, June 21, 2016

TAARIFA KWA WAFANYAKAZI WA MAKAO MAKUU, JNIA NA BANDARINI.




YAH: KUSIKILIZA KERO NA KUPOKEA MAONI MBALIMBALI YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI.
Mkurugenzi Mkuu ameandaa siku ya Jumatano saa 7 mchana Tarehe 22 Juni 2016 ili kusikiliza matatizo sambamba na kupokea maoni mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini. Kazi hii itatolewa katika ukumbi wa Mikutano, ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza-Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kazi hii ni utekelezaji wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini kwa mwaka 2016. 
IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO- MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA





YAH: KUSIKILIZA KERO NA KUPOKEA MAONI MBALIMBALI YA WANANCHI KUHUSU HUDUMA ZA HALI YA HEWA NCHINI.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imeandaa siku ya Alhamis, saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana, Tarehe 23 Juni 2016 ili kusikiliza kero sambamba na kupokea maoni mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini. Kazi hii  itafanyika katika ukumbi wa Mikutano, ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza-Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kazi hii ni utekelezaji wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini kwa mwaka 2016. 
‘Wananchi wote mnakaribishwa’
IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO- MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Friday, June 17, 2016

MKUTANO WA SITINI NA NANE WA KAMATI KUU YA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WMO-EXCECUTIVE COUNCIL-68), GENEVA, USWISI, TAREHE 15-24 JUNI, 2016



Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa,Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Mjumbe wa “WMO Excecutive Council” na Bw. Wilbert Timiza Muruke, Meneja Mahusiano ya Kimataifa wa TMA katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Excecutive Council-68) unaondelea, Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 15-24 Juni 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi alikuwa miongoni mwa wajumbe 37 wa Mkutano wa Sitini na Nane wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization Executive Council WMO-EC 68) unaofanyika makao makuu ya Shirika hilo, Geneva nchini Uswisi kuanzia tarehe 15 hadi 24 Juni, 2016. Pia Dkt. Kijazi anaingia katika Kamati Kuu ya WMO akiwa kati ya wanawake wawili (2) kutoka Afrika na watano (5) kati ya thelathini na saba (37) kuwakilisha Dunia nzima.
Mkutano wa WMO-EC-68 pamoja na masuala mengine unajadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Duniani sambamba na kutimiza Makubaliano ya Kikanda na Kimataifa katika kukabiliana na athari zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
Aidha masuala yanayojadiliwa ni sehemu ya Mpango Mkakati wa WMO na vipaumbele vyake katika kipindi cha mwaka 2015-2019 unaojumuisha utekelezaji wa programu za utoaji wa huduma bora zaidi za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for Climate Services”, Utekelezaji wa programu ya uboreshaji wa vituo vya upimaji wa hali ya hewa na ubadilishanaji wa data za hali ya hewa “WMO Integrated Global Observing System and Information System (WIGOS/WIS), utoaji wa tahadhari za mapema ili kukabiliana na maafa “Disaster Risk Reduction, Resilience and Prevention”, Uboreshaji wa huduma za usalama na usafiri wa anga “Aviation meteorological services”, Kuboresha huduma za hali ya hewa kwa maeneo ya Dunia yenye barafu ya asili ikiwa ni pamoja na milima mirefu kama Kilimanjaro “Polar and high mountain regions”, Kujenga uwezo wa rasilimali watu na vitendea kazi hasa kwa nchi zinazoendelea na visiwa vidogo na tafiti za hali ya hewa. Aidha Mkutano huu unajadili pia namna ya kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa kama njia ya kuboresha huduma za hali ya hewa kote duniani na kutatua changamoto za athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi na uhifadhi wa mazingira.
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI-AFISA UHUSIANO TMA


Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...