Tuesday, May 3, 2016

MAFUNZO UTANGAZAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA WANAHABARI WA KITUO CHA AZAM

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeendelea kutoa mafunzo ya hali ya hewa kwa wanahabari ili kuwajengea uwezo wanahabari kuelimisha jamii juu ya umuhimu na matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi amefungua rasmi mafunzo ya wiki tatu ya hali ya hewa kwa ajili ya watangazaji na watayarishaji vipindi vya Azam Media. Mafunzo hayo yanatolewa na Mamalaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Shirika la Hali ya Hewa Duniani WMO

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwawezesha watangazaji na watayarishaji wa vipindi kuwa na uelewa wa masuala ya hali ya hewa ili kufikisha taarifa hizo katika lugha rahisi lakini inayowakilisha taarifa hizo kadri ilivyokusudiwa. Mafunzo hayo ya wiki tatu  yanatarajiwa kumalizika tarehe 20 mwezi Mei mwaka huu.

No comments:

Post a Comment