Friday, May 6, 2016

LONGIDO NA KITETO WAENEZA ELIMU YA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Ladislaus Chang'a akifungua warsha ya wadau inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bw. Laurent Shauri akimkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha ya wadau inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Maafisa kilimo kutoka Wilaya ya Kiteto na Longido wakielezea namna walivyonufaika na elimu kutoka TMA katika warsha ya wadau inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Meza kuu pamoja na wadau mbalimbali wakiendelea kupata uzoefu katika warsha ya wadau inayohusu kuimarisha usambazaji na matumizi ya taarifa na huduma zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

Na: Monica Mutoni


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Wilaya za Longido na Kiteto katika kuhakikisha matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa yanafanyika sambamba na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. TMA imetumia uzoefu wa Kiteto na Longido ili kuimarisha huduma katika maeneo mengine ya nchi yetu, wakati ilipoandaa warsha iliyowakusanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo na mifugo. Warsha hiyo ilifanyika tarehe 04 Mei 2016, Blue Pearl, Dar es Salaam.
Juhudi hizi zinafanyika kwa kushirikiana na mpango malumu wa kidunia (Global Frameworks for Climate Services (GFCS)) wa kuimarisha  utoaji na usambazaji wa taarifa za hali ya  hewa  ili kuongeza tija na ufanisi katika shughuli za uzalishaji na maendeleo na pia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mpango huu umefadhiliwa na Serikali ya Norway.
 Utekelezaji wa mpango wa GFCS umelenga Wilaya za Kiteto na Longido ambazo ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika na mabadiliko ya hali ya hewa na ikaonekana ni muhimu mradi huu ufike maeneo ambayo yana mahitaji ya taarifa za hali ya hewa hasa kwa wakulima na wafugaji wanaoishi pembezoni mwa Tanzania.
Mabadiliko ya hali ya hewa yamejidhihirisha sana hasa katika kubadilika kwa mtawanyiko wa mvua, misimu ya mvua kuwa mifupi, kupungua kwa wingi wa mvua na kuongezeka kwa joto.


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...