Tuesday, April 26, 2016

WAFANYAKAZI WA TMA WATAKIWA KWENDA NA WAKATI

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wametakiwa kuachana na mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi katika kuhifadhi taarifa zao muhimu na badala yake kuanza  kutumia mfumo wa kisasa wa kieletroniki.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Pof. Makame Mbarawa  jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wafanyakazi hao na kueleza kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kununulia karatasi.

“Katika ofisi zenu nimeona kila mtu anakomputa ni jambo zuri hivyo zitumieni katika kuhifadhi taarifa muhimu za taasisi yenu kwa mfumo wa kieletroniki,” alisema Prof.Mbarawa.

 Aliongeza kwa kusema kuwa serikali imetumia fedha nyingi katika kujenga mkongo wa taifa wa kuhifadhi taarifa muhimu  hususani za serikali pamoja na taasisi zake hivyo ni budi  waanze kuutumia mkongo huo kwa kuhifadhia taarifa zao.

Pia amewataka watumishi kuwa waadilifu,wachapaka kazi, wabunifu na kuwa na uwazi baina ya watendaji wa juu na watumishi wa ngazi ya chini kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa mikoani.

“Watanzania wanamatarajio mengi kutoka kwetu  katika kukuza uchumi wa nchi hivyo ni wajibu wetu kutimiza matarajio yao kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwemo miundo mbinu imara ya barabara, bandari ,shirika la ndege la kisasa na utabiri  wa hali ya hewa wenye uhakika,” alisema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa  alitoa wito kwa kuwataka  watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano  kila mmmoja kujituma katika eneo lake la kazi ili kuleta matokeo yaliyobora na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kufikia uchumi wa kati.

Na Lorietha Laurence – Maelezo

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...