Tuesday, April 26, 2016

WAFANYAKAZI WA TMA WATAKIWA KWENDA NA WAKATI

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wametakiwa kuachana na mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi katika kuhifadhi taarifa zao muhimu na badala yake kuanza  kutumia mfumo wa kisasa wa kieletroniki.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Pof. Makame Mbarawa  jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wafanyakazi hao na kueleza kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kununulia karatasi.

“Katika ofisi zenu nimeona kila mtu anakomputa ni jambo zuri hivyo zitumieni katika kuhifadhi taarifa muhimu za taasisi yenu kwa mfumo wa kieletroniki,” alisema Prof.Mbarawa.

 Aliongeza kwa kusema kuwa serikali imetumia fedha nyingi katika kujenga mkongo wa taifa wa kuhifadhi taarifa muhimu  hususani za serikali pamoja na taasisi zake hivyo ni budi  waanze kuutumia mkongo huo kwa kuhifadhia taarifa zao.

Pia amewataka watumishi kuwa waadilifu,wachapaka kazi, wabunifu na kuwa na uwazi baina ya watendaji wa juu na watumishi wa ngazi ya chini kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa mikoani.

“Watanzania wanamatarajio mengi kutoka kwetu  katika kukuza uchumi wa nchi hivyo ni wajibu wetu kutimiza matarajio yao kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwemo miundo mbinu imara ya barabara, bandari ,shirika la ndege la kisasa na utabiri  wa hali ya hewa wenye uhakika,” alisema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa  alitoa wito kwa kuwataka  watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano  kila mmmoja kujituma katika eneo lake la kazi ili kuleta matokeo yaliyobora na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kufikia uchumi wa kati.

Na Lorietha Laurence – Maelezo

Monday, April 25, 2016

MHE. PROF. MAKAME MBARAWA AAGIZA MENEJIMENT NA WATUMISHI WA TMA KUWA WAADILIFU NA WABUNIFU KATIKA UTEKELEZAJI WA KAZI ILI KUFIKIA MALENGO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO IFIKAPO MWAKA 2025

Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akipokelewa na menejimenti ya TMA na kusaini kitabu cha wageni
Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kitengo cha Data (Takwimu za taarifa za hali ya hewa )
Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kitengo cha Hali ya Hewa Kilimo.

Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kitengo cha Huduma za Utabiri
.
Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza na menejimenti na wafanyakazi wa TMA

Sunday, April 24, 2016

BODI YA USHAURI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA YASISITIZA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA KUZINGATIA MAADILI, KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI KWA WATUMISHI WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA


Katika jitihada za kuhakikisha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inafikia viwango vya kimataifa kulingana na matakwa ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma kimefanikiwa kufanya awamu ya tatu ya  kozi ya huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga kwa baadhi ya wafanyakazi wa TMA.

Akifunga rasmi kozi hiyo na kuwatunuku vyeti wahitimu, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi aliwataka wahitimu wote pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka kuwa vielelezo katika vituo vyao vya kazi katika kuzingatia maadili, kanuni na taratibu za kazi na kufanya kazi kwa weledi mkubwa hususani kwenye sekta ya usafiri wa anga. Aidha aliahidi kwamba Bodi itashirikiana na menejimenti ya TMA kuhakikisha kwamba miundo mbinu ya Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma inaboreshwa.

Akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Agnes Kijazi, Mkuruggenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa alisema mafunzo hayo ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa Mamlaka wa kuendeleza watumishi ili kukidhi viwango vya Shirika la Hali ya Hewa Duniani.

Naye Mkuu wa Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma, Bw. Joseph Aliba alitoa shukrani za dhati kwa serikali kwa kuwezesha uboreshaji wa huduma kama vile usajili wa chuo, maktaba, ujenzi wa uzio wa chuo, mafunzo kwa waalimu, kuunganishwa katika mkongo wa Taifa huku akitaja baadhi ya changamoto zilizopo.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wote, Bi. Beatrice Kitero, alishukuru Mamlaka kwa mafunzo na kuahidi kuyafanyia kazi katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa kwaajili ya usafiri wa anga nchini.

Kozi ya huduma za hali ya hewa kwaajili ya usafiri wa anga, imeandaliwa na Chuo cha Hali ya Hewa  Kigoma kwa muda wa mwezi mmoja na ilifanyika Makao Makuu ya TMA, Ubungo Plaza, Dar es Salaam. Wahitimu ni wafanyakazi wa Mamlaka waliohitimu degree ya Hali ya Hewa kutoka vituo vya Mbeya, Dodoma, Kigoma, Makao Makuu (DSM) na Zanzibar.Monday, April 18, 2016

GFCS IMPLEMENTATION:SECOND PDT EXTRAORDINARY MEETING HELD AT TMA-HQ, UBUNGO PLAZA


GFCS:WEATHER AND CLIMATE SERVICES AWARENESS AT LONDIDO DISTRICT

TMA staff in collaboration with partners representative of the Longido District Authorities continuing with GFCS implementation in four villages of Olmong, lelang'wa,Ilkarso and Kamwanga. The team also conducted awareness to around 600 students at Enduimet Secondary School in Longido.