Tuesday, March 31, 2015

KAIMU MKUU WA MKOA WA MOROGORO AFUNGUA RASMI BARAZA LA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI MKOANI MOROGORO

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Festo Kiswaga (Mkuu wa Wilaya ya Mvomero)  akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa TMA linalofanyika mkoani Morogoro katika hoteli ya Oasis tarehe 31 Machi hadi 01 Aprili 2015.



Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt Agnes Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua Baraza la wafanyakazi wa TMA linalofanyika mkoani Morogoro katika hoteli ya Oasis tarehe 31 Machi hadi 01 Aprili 2015.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa TMA linalofanyika mkoani Morogoro katika hoteli ya Oasis tarehe 31 Machi hadi 01 Aprili 2015 katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, wa kwanza kulia ni katibu wa baraza bw. Chuki Sangalugembe.

Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa TMA wakiwakumbuka baadhi ya wafanyakazi waliofariki katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa TMA linalofanyika mkoani Morogoro katika hoteli ya Oasis tarehe 31 Machi hadi 01 Aprili 2015 wakimsikiliza mgeni rasmi mhe. kaimu mkuu wa mkoa

Wednesday, March 25, 2015

UFUNGUZI WA WARSHA YA WADAU KUHUSU “HUDUMA ZITOLEWAZO NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NA UAINISHAJI WA MAHITAJI YA WADAU”, HOTELI YA BLUE PEARL, DAR ES SALAAM, TANZANIA, TAREHE 24 MACHI, 2015

Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uanishaji wa matakwa ya wadau,Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam, Tarehe 24 Machi 2015.

Mkurugenzi wa Huduma za Utafiti na Matumizi TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa ufafanuzi kwenye warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewaza na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uanishaji wa matakwa ya wadau,Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam, Tarehe 24 Machi 2015.

Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi wa Huduma za Utafiti na Matumizi TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Dkt. Hamza Kabelwa katika ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewaza na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uanishaji wa matakwa ya wadau,Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salam, Tarehe 24 Machi 2015.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewaza na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uanishaji wa matakwa ya wadau,Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam, Tarehe 24 Machi 2015.
 Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na  washiriki wa warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewaza na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uanishaji wa matakwa ya wadau,Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam, Tarehe 24 Machi 2015.

Sunday, March 22, 2015

MAELEZO YA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA DKT. AGNES L. KIJAZI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI TAREHE 23 MACHI 2015



Tarehe ya 23 Machi kila mwaka Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kushirikiana na wadau mbali-mbali huadhimisha siku ya hali yahewa  Duniani. Maadhimisho haya ni kumbukumbu ya siku ya kuanzishwa kwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani tarehe 23 Machi, 1950. Katika kusherehekea siku hii Shirika la Hali ya Hewa Duniani hutoa kauli-mbiu inayotumika na nchi zote wanachama.  Kauli-mbiu ya mwaka huu ni “Uelewa wa Hali ya Hewa kwa maamuzi stahiki” (Climate Knowledge for Climate Action).  Kauli mbiu hii inalenga kutambua umuhimu wa kuhusisha masuala ya hali ya hewa katika shughuli  za maendeleo za kijamii na kiuchumi  hususan katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa (climate change). Maarifa ya hali ya hewa ambayo yamejengeka katika miongo kadhaa iliyopita ni mchango mkubwa sana na rasilimali kubwa katika kufanya maamuzi stahiki ya matumizi ya taarifa za hali ya hewa.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilianzishwa kwa sheria ya wakala wa serikali Na. 30 ya mwaka 1997 na kuzinduliwa rasmi mwezi Desemba 1999. Mamlaka inafanya kazi zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na inaiwakilisha  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Shirika hilo. Tanzania kupitia TMA inaadhimisha siku hii ya hali ya hewa duniani kwa kusherehekea mafanikio yaliyofikiwa na WMO tangu kuanzishwa kwake na Mafanikio ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa hapa nchini.

 Miongoni mwa majukumu ya TMA ni pamoja na kufanya shughuli za uangazi, kukusanya na kuhifadhi  data na takwimu za hali ya hewa, kutoa utabiri wa hali ya hewa na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa hapa nchini na nje ya nchi. TMA pia inaiwakilisha Tanzania katika masuala ya hali ya hewa kimataifa na  pia Mamlaka  inashirikiana na wadau wengine hapa nchini na katika kanda ya Afrika mashariki na kusini mwa Afrika ili kuboresha utabiri wa hali ya hewa wa msimu ambao ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Tunaposherekea siku ya hali ya hewa Duniani, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajitahidi kutoa huduma za hali ya hewa za kuaminika, zinazotolewa kwa wakati, zenye viwango vya usahihi vinavyokubalika na katika lugha rahisi na ya kueleweka ili kukidhi mahitaji ya jamii ikiwa ni pamoja na watoa maamuzi na hivyo kuchangia katika maendeleo ya Taifa. Mfano mzuri wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa  katika kufanya maamuzi ni katika sekta ya kilimo na usafiri wa Anga. Uelewa wa kuanza, kuisha na urefu wa msimu wa mvua ni muhimu katika kufanya maamuzi ya shughuli za kilimo kama vile, wakati gani wa kupanda na kuvuna, pia aina gani ya mazao yanaweza kupandwa , wakati gani wa kunyunyizia dawa na namna gani ya kuhifadhi mazao.  Katika Usafiri wa anga taarifa za hali ya hewa ni muhimu wakati wa kutua, kupaa na usafiri wa ndege inapokuwa angani. Aidha, taarifa za hali ya hewa zinatumika kibiashara na wamiliki wa ndege katika kujua kiasi cha mafuta yanayohitajika na kiasi cha mzigo unaoweza kubebwa katika safari husika.
Maeneo mengine ambayo taarifa za hali ya hewa ni za muhimu ni katika ujenzi, mipango miji pamoja na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi.  Taarifa za hali ya hewa husaidia wahandisi na maafisa mipango miji kuainisha maeneo ya kuweka miundombinu mbalimbali ikiwemo ya mifumo ya maji safi na  maji taka, ujenzi wa  madaraja n.k.  Takwimu za vimbunga na mfumo wa upepo katika ukanda wa Pwani ni muhimu sana katika shughuli zinazoendelea za utafiti na uchimbaji wa mafuta. Idadi ya siku ambazo mvua itanyesha na hali ya joto ya mahali husika ni muhimu katika sekta ya utalii. Taarifa za matukio ya hali mbaya ya hewa kama vile mafuriko na ukame, upepo mkali pamoja na mvua ya mawe na kujua eneo litakalo athirika ni muhimu sana katika mipango mbalimbali ya maendeleo.
Hii ni baadhi ya mifano michache tu ambapo uhitaji na uelewa wa huduma za hali ya hewa hauepukiki. Katika kuhakikisha kuwa jamii yetu inafikiwa na huduma hizi muhimu za hali ya hewa, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) husambaza taarifa hizi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kama vile, Facebook, Twitter, YouTube.
Kutokana na kuongezeka uelewa wa sayansi ya hali ya hewa, utabiri wa hali ya hewa umeendelea kuongezeka viwango vya usahihi na hivyo nashauri sekta zote za kiuchumi na kijamii hapa nchini kuendelea kutumia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa  katika kupanga mipango yao ya muda mfupi na mrefu. Endapo utabiri wa hali ya hewa utolewao na TMA utazingatiwa na kutumiwa kwa makini utasaidia sana katika kupunguza athari za majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa .  Adha, ikumbukwe kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa kuokoa maisha na kupunguza hasara ya upotevu wa mali kwa kuwa na matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa.

TMA imepata cheti cha ubora cha kimataifa (ISO 9001:2008) katika utoaji wa huduma  bora za hali ya hewa kwa usafiri wa anga. Cheti hiki kilipatikana mwaka 2011 na hii ni sifa kwa nchi yetu hasa ikikumbukwa kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kupata cheti hicho kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.  Mipango iko mbioni kuhakikisha huduma zitolewazo na TMA katika sekta zote zinasajiliwa na shirika la viwango duniani.  Hivyo tunaposherehekea siku ya hali ya hewa Duniani naendelea kuwashauri watanzania wenzangu katika sekta zote za kiuchumi na kijamii kutumia taarifa za hali ya hewa kwa maendeleo endelevu ya taifa letu. Nawatakia maadhimisho mema ya siku ya hali ya hewa duniani mwaka huu wa 2015
Uelewa wa Hali ya Hewa kwa maamuzi stahiki


Friday, March 20, 2015

WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. SAMUEL SITTA AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUISHAWISHI JAMII JUU YA UELEWA WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA



Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta pamoja na Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Kijazi wakijadili jambo wakati wa mkutano na wanahabariakiongea na wanahabari kwenye maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani tarehe 23 Machi 2015
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Samuel Sitta (MB) akiongea na wanahabari kwenye maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani yanayofanyika kila ifikapo Tarehe 23 Machi, yenye kauli mbiu isemayo 'Uelewa wa hali ya hewa kwa maamuzi stahiki'. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu TMA, Dkt. Agnes Kijazi. (Picha Juu)

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...