Wednesday, September 9, 2015

TANZANIA YAANDAA MAFUNZO YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA ULINZI KWA NCHI YA KUSINI MWA AFRIKA.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),Dkt.Agnes Kijazi amefungua rasmi mafunzo ya utunzaji wa mazingira na ulinzi kwa nchi za Kusini mwa Afrika. Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Dkt. Kijazi, Kaimu Mkutugenzi Mkuu Dkt. Pascal Waniha alielezea kwa kina uhusiano uliopo kati ya hali ya hewa na mazingira, hivyo utunzaji wa mazingira ni chachu katika maendeleo endelevu ya nchi zetu. ‘Ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa mkubwa kati ya hali ya hewa na mazingira yetu hivyo kuchangia katika kuimarisha uhusuiano wake kwa maendeleo endelevu ya nchi zetu,.Alisema Dkt.Kijazi.
Aidha aliwashukuru wadhamini wa mradi na mafunzo kwa kuendelea kuchangia katika uborshaji wa huduma za hali ya hewa nchini za Kusini mwa Afrika  hususan Tanzania. ‘Umoja wa Ulaya kupitia Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika  wameendelea kuisaidia Tanzania kwa njia mbalimbali kama vile  taarifa za ukame (TMA), madhara ya moto (Wizara ya Utalii), taarifa za kilimo (Wizara ya Kilimo), Mafuriko (Kitengo cha Maafa) na usalama wa bahari ya Hindi (TAFIRI)  vilevile  usimikaji wa vifaa na uwezekano wa TMA kutumia satelaiti za Ulaya katika uchambuzi wa taarifa za hali ya hewa. Kwa kupitia hayo yote Tanzania  imezidi kuboresha usahihi wa  huduma zake hivyo kusaidia kupunguza athari kwa mazingira yetu sambamba na kujiandaa kukabiliana na athari hizo’.Aliongezea Dkt. Kijazi.

Tanzania imeandaa mafunzo hayo ya siku tano  yaliyofanyika tarehe 7 hadi 11 Septemba 2015 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Kilimo na Usalama wa Chakula,TMA, Taasisi ya Misitu,TAFIRI, Kitengo cha Maafa, Chuo cha Ardhi na wadau mbalimbali. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalam kutoka Tanzania, Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Namibia na Botswana. Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa ziko sahihi kwa utoaji maamuzi ya  maendeleo ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA : MONICA MUTONI, AFISA UHUSIANO,MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

No comments:

Post a Comment