Friday, September 25, 2015

MAKAMU WA RAIS AITAKA TMA KUTOA TAHADHARI ZA HALI YA HEWA KATIKA MAENEO MADOGOMADOGO NCHINI


Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Gharib Bilal akipata maelezo ya huduma za hali ya hewa majini kutoka kwa maafisa wa TMA Bi. Monica Mutoni (Afisa Uhusiano) na Bw. Daud Amasi (Meneja Kanda ya Kusini) kwenye maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, mkoani Mtwara. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Halima Dendego (mwenye kofia)
Baadhi ya wadau wa sekta ya bahari nchini wakipata elimu ya hali ya hewa katika maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika mkoani Mtwara tarehe 20-22 Septemba 2015.

Wednesday, September 9, 2015

TANZANIA YAANDAA MAFUNZO YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA ULINZI KWA NCHI YA KUSINI MWA AFRIKA.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),Dkt.Agnes Kijazi amefungua rasmi mafunzo ya utunzaji wa mazingira na ulinzi kwa nchi za Kusini mwa Afrika. Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Dkt. Kijazi, Kaimu Mkutugenzi Mkuu Dkt. Pascal Waniha alielezea kwa kina uhusiano uliopo kati ya hali ya hewa na mazingira, hivyo utunzaji wa mazingira ni chachu katika maendeleo endelevu ya nchi zetu. ‘Ni matarajio yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa mkubwa kati ya hali ya hewa na mazingira yetu hivyo kuchangia katika kuimarisha uhusuiano wake kwa maendeleo endelevu ya nchi zetu,.Alisema Dkt.Kijazi.
Aidha aliwashukuru wadhamini wa mradi na mafunzo kwa kuendelea kuchangia katika uborshaji wa huduma za hali ya hewa nchini za Kusini mwa Afrika  hususan Tanzania. ‘Umoja wa Ulaya kupitia Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika  wameendelea kuisaidia Tanzania kwa njia mbalimbali kama vile  taarifa za ukame (TMA), madhara ya moto (Wizara ya Utalii), taarifa za kilimo (Wizara ya Kilimo), Mafuriko (Kitengo cha Maafa) na usalama wa bahari ya Hindi (TAFIRI)  vilevile  usimikaji wa vifaa na uwezekano wa TMA kutumia satelaiti za Ulaya katika uchambuzi wa taarifa za hali ya hewa. Kwa kupitia hayo yote Tanzania  imezidi kuboresha usahihi wa  huduma zake hivyo kusaidia kupunguza athari kwa mazingira yetu sambamba na kujiandaa kukabiliana na athari hizo’.Aliongezea Dkt. Kijazi.

Tanzania imeandaa mafunzo hayo ya siku tano  yaliyofanyika tarehe 7 hadi 11 Septemba 2015 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Kilimo na Usalama wa Chakula,TMA, Taasisi ya Misitu,TAFIRI, Kitengo cha Maafa, Chuo cha Ardhi na wadau mbalimbali. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalam kutoka Tanzania, Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Namibia na Botswana. Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha taarifa zinazotolewa ziko sahihi kwa utoaji maamuzi ya  maendeleo ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA : MONICA MUTONI, AFISA UHUSIANO,MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

TANZANIA CONDUCTS MONITORING FOR ENVIRONMENT AND SECURITY IN AFRICA (MESA) - SADC TRAINING



The Tanzania Meteorological Agency Director General Dr. Agnes Kijazi officiate a Tanzania Monitoring of Environment and Security in Africa (MESA) training for SADC region. During her official speech read by Acting Director General Dr. Pascal Waniha, she pointed out the relationship between meteorology and environment for our countries sustainable development. ‘I hope this training workshop will enhance our knowledge base and strengthen our long-term collaboration on issues related to Meteorology and Environment for sustainable development of our Country’. She said
She also thanks the sponsors for supporting the project as well as monitoring the implementation of the facilities provided and installed. ‘The European Union (EU) through Africa Union Commission (AUC) and SADC- has continued with their support to the Government of Tanzania in the four services which are Drought performed by the  Meteorological Agency (TMA),  Fire service in the Ministry of Natural Resources and Tourism ( MNRT) , Agriculture service within the Ministry of Agriculture, Food Security and Cooperatives (MAFC) and Floods service hosted by the Disaster Management Department (DMD) at the Prime Ministers Office. With  this support , Tanzania Indian Ocean marine and the MESA-Indian Ocean Commission (IOC) to the Tanzania Fisheries and Research  Institute (TAFIRI). This EU-AUC  support through SADC is being implemented  through various initiatives, which include the support by European Meteorological Satellites (EUMETSAT). These have been very useful to various governments  and private sectors,    Accurate forecast and early warning information prior to an event on environmental hazards is very important for preparedness’.  She added.


The 5 days national training workshop will take place from 7 to 11 September 2015 in Tanzania which consists of various environmental national stakeholders from MNRT, MAFC, TMA, TAFIRI, Tanzania Forest Research Institute (TAFORI), DMD,   Ardhi University and collaborating partners.  The training is being conducted by the national MESA-SADC Tanzania services Focal Points experts supported by technical Experts from Zimbabwe University, Namibia Polytechnic University and from Botswana University of Agriculture and Natural Resources. The objective of the training is to ensure that products and information obtained through Earth Observation are well-packed understood for supporting the decision-makers in their various related activities.


RELEASED BY: MONICA MUTONI, COMMUNICATION OFFICER, TANZANIA METEOROLOGICAL AGENCY

Wednesday, September 2, 2015

TMA YATOA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2015 KUPITIA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa utabiri wa msimu kwa miezi ya Septemba hadi Desemba 2015 kwa wanahabari.kushoto kwa Dkt, Kijazi ni mkurugenzi wa huduma za utabiri, Dkt. Hamza Kabelwa.

Meneja Kitengo cha Utabiri Bw. Samuel Mbuya (aliyesimama) akitoa ufafanuzi nwa kina kuhusiana na EL NINO kwa wanahabari  
Wanahabari wakiwa kazini tayari kwa kueleimisha umma kuhusiana na utabiri uliotolewa na TMA.



Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa iliyopo na inayotarajiwa, mvua za vuli zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:

(i)     Mvua za vuli (kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)
Msimu wa mvua wa miezi ya Oktoba hadi Disemba (vuli) ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani kwa maeneo mengi. Mvua hizo zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki mbili za mwisho za mwezi Septemba 2015 katika  kanda ya ziwa Victoria na katika maeneo machache ya Pwani ya kaskazini.

Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga): Mvua zinatarajiwa kuanza  kati ya wiki ya tatu ya mwezi  Septemba 2015 katika mikoa ya Kagera na Mara na kusambaa katika Mikoa mingine. Mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo hayo.

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro,  mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba):
Mvua zinatarajiwa  kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2015 na zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani  hadi wastani katika mikoa  ya Tanga, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba; na wastani hadi juu ya wastani katika maeneo wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza  ya mwezi Oktoba , 2015 katika Mkoa wa Arusha na kusambaa katika mikoa mingine na zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani kwa ujumla.

(ii)        Mvua za Msimu (Novemba – Aprili) kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua.
Msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili ni mahususi kwa maeneo ya  Magharibi mwa nchi(Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa), kanda ya  kati (Mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini-Magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro), kusini mwa nchi na pwani ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara) zinatarajiwa kuanza mwezi Novemba 2015.  Mvua katika maeneo mengi zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani. Hata hivyo, maeneo machache ya mikoa iliyo kusini zaidi mwa nchi yanatarajiwa kupata mvua za chini wastani kama ifuatavyo;


Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa):
Mvua za msimu zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Rukwa na Katavi. Kaskazini mwa mikoa ya Tabora na Kigoma (Wilaya ya Kibondo) kunatarajiwa kuwa na mvua za juu ya wastani hadi za wastani. Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2015.

Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma):
Mvua za msimu zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na tatu ya mwezi Novemba na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Singida na Dodoma. Hata hivyo maeneo ya kaskazini mwa mikoa ya Dodoma na Singida yanatarajiwa kuwa na mvua za juu ya wastani hadi wastani.

Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Hata hivyo kusini mwa mkoa wa Njombe na baadhi ya maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro (Mahenge) mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa.

Maeneo ya kusini na pwani ya kusini (Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara)
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba 2015 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi.  Hata hivyo maeneo machache ya upande wa mashariki mwa mikoa ya Lindi na Mtwara yanatarajiwa kupata mvua  za wastani hadi juu ya wastani. 




Izingatiwe kuwa pamoja na kuwapo kwa uwezekano wa matukio ya mvua kubwa katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua juu ya wastani, hali hiyo pia inaweza kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Matukio ya Vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa bahari ya Hindi yanatarajiwa kuchangia katika mwenendo wa mvua hapa nchini.


Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...