Wednesday, July 1, 2015

WARSHA YA KISAYANSI KUHUSU HUDUMA ZA HALI YA HEWA KUPITIA MODELI YA ‘PRECIS’, KUANZIA TAREHE 29 JUNI HADI 3 JULAI 2015, DAR ES SALAAM, TANZANIA.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) wameandaa  mafunzo ya hali ya hewa kwa kutumia modeli ya PRECIS (Providing Regional Climates for Impact Studies) kuanzia tarehe 29 Juni hadi 03 Julai 2015. Warsha/ mafunzo haya yameandaliwa na TMA chini ya mwamvuli wa mradi wa GFCS unaotekelezwa kwa upande wa Afrika katika nchi za Tanzania na Malawi

Washiriki wa mafunzo hayo kutoka TMA na Kurugenzi ya Hali ya Hewa ya Malawi  wanategemea kujifunza matumizi ya modeli ya PRECIS kutoka kwa mtaalamu kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambayo imekuwa ikitumia modeli hiyo katika utekelezaji wa huduma za hali ya hewa.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa wa utoaji huduma za hali ya hewa pamoja na kuweza kutoa taarifa sahihi za muda mrefu zenye kuweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi. Alisema Dkt.Kijazi

PRECIS ni mfumo unaweza kutoa taarifa za hali ya hewa za muda mrefu (Klimatolojia) kwa eneo husika. 

Imetolewa na Monica Mutoni, Afisa Uhisiano. TMA
No comments:

Post a Comment