Wednesday, July 8, 2015

WANASAYANSI WA HALI YA HEWA WAKUTANA KUHAMASISHANA KUFANYA TAFITI ZENYE KULETA TIJA KWA MAENDELEO YA NCHI.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi akiwa katika picha ya pamoja  na wanasayansi ya hali ya hewa (meteorologists) kutoka Makao Makuu na JNIA TMA.

Wanasayansi ya hali ya hewa (Meteorologists) wamekutana katika warsha ya siku moja iliyofanyika tarehe 06 Julai 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA). Warsha hiyo ambayo ulikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali yakiwemo kubobea (specialization) katika matumizi ya sayansi ya hali ya hewa kwenye sekta mbalimbali kama vile kilimo, afya, nishati, maji, usafiri wa anga na kwenye maji n.k; ushiriki wa TMA katika kuchangia masuala ya hali ya hewa ya kikanda na kimataifa, na wataalam kujikita katika tafiti zenye kuchangia katika maendeleo ya taifa letu.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA  Dkt. Agnes Kijazi alisema dhumuni ni kuangalia changamoto zinazokabili sayansi ya hali ya hewa hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi hivyo basi kuangalia jinsi ya kuboresha taaluma ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja  na kufanya tafiti zenye tija kwa maedeleo ya nchini yetu. Aidha alielezea pia umuhimu wa kubobea (specialization) kwenye utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa sekta zingine.

Dkt Kijazi aliongeza kwa kusema, warsha kama hizi ni fursa nzuri  kwa wanasayansi kutambua nafasi zao na mchango wao wa kutoa  huduma bora za hali ya hewa kwa jamii.

Warsha hiyo imeandaliwa katika mpango wa TMA kuboresha huduma zake ili kufikia dira waliyojiwekea ya kuwa kitovu cha ubora cha utoaji huduma za hali ya hewa ‘Centre of excellence in provision of meteorological services’
 Dkt. Agnes Kijazi akisisitiza jambo kwa wanasayansi katika warsha ya siku moja ya wataalamu hao.
Baadhi ya wanasayansi ya hali ya hewa kutoka Makao Makuu ya TMA na ofisi za JNIA wakimsikiliza kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mkuu. 

Imetolewa na :Monica Mutoni, Ofisi ya Uhusiano- Mamlaka ya Hali ya Hewa


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...