Monday, June 29, 2015

BWANA WILBERFORCE KAHWA KIKWASI ATUNUKIWA NISHANI YA “UTUMISHI MREFU, MAADILI MEMA NA UBUNIFU DARAJA LA PILI” NA MTUKUFU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETEBwana Wilberforce Kahwa Kikwasi (Mtabiri mwandamizi na msimizi mkuu wa shughuli za uchambuzi na uandaaji wa utabiri wa hali ya hewa-Senior Meteorologist and Head-Analyst Incharge) kituo kikuu cha utabiri wa hali ya hewa Tanzania, mnamo tarehe 23 Juni 2015, katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu, alitununikiwa nishani ya “Utumishi Mrefu, Maadili Mema na ubunifu Daraja la Pili” na Mtukufu rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete”.
Nishani hii ni heshima kubwa kutoka kwa mtukufu rais kwa kutambua mchango wa Bwana Wilberforce Kahwa Kikwasi na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa ujumla katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa kwa kufanyakazi kwa uvumilivu, juhudi na weledi katika kutatua matatizo mbalimbali.
Bwana Wilberforce Kahwa Kikwasi amekuwa mbunifu kwa kubuni mfumo kielektroniki wa ukusanyaji na mawasiliano ya taarifa na takwimu za hali ya hewa (Digital Meteorological Observatory) ambao unaboresha huduma za hali ya hewa na kupunguza gharama za uendeshaji.
Bodi ya ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (MAB), Menejimenti na wafanyakazi wote tunampongeza Bwana Wilberforce Kahwa Kikwasi kwa heshima hiyo kubwa aliyoipata ambayo ni heshima kwetu sote.
Hivyo basi nishani hii iwe chachu kwa watumishi wote wa TMA katika kujituma, kushirikiana, uvumilivu na kuwa na ubunifu. Kubwa zaidi tudumishe mshikamano wetu ambao ndio siri kubwa ya mafanikio yetu.
“Hali ya Hewa kwa maendeleo endelevu”


IMETOLEWA NA:
MONICA MUTONI
AFISA MAHUSIANO,
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

No comments:

Post a Comment