Monday, May 4, 2015

WARSHA YA WAKUU WA TAASISI ZINAZOMILIKI VITUO VYA HALI YA HEWA NCHINI YAFANYIKA MJINI ARUSHA

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, mkurugenzi wa Kitengio cha Maafa Brigedia Jenerali Mbazi Msuya ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha ya wakuu wa taasisi wanaomiliki vituo vya hali ya hewa nchini, iliyofanyika Arusha katika hoteli ya Kibo Palace tarehe 30 Aprili 2015.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania  (TMA)  Dkt. Agnes Kijazi na kushoto kwake ni mwakilishi kutoka Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Elijah Mukhala
Mwezeshaji Bw. Augustine Kanemba akimkaribisha mwakilishi kutoka WMO, Dkt. Elijah Mukhala kutoa nasaha zake katika warsha hiyo.
Mkurugenzi Mkuu TMA akitoa hotuba fupi wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuhutubia wanawarsha
Mgeni rasmi Brigedia jenerali Mbazi Msuya akihutubia wakuu wataasisi zinazomiliki vituo vya hali ya hewa wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya wanawarsha wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha waliokaa kutoka kulia kwa mgeni rasmi ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Kijazi, mkurugenzi kitengo cha usalama wa chakula, Kilimo Bw. Ombaeli Lemweli na mkurugenzi mkuu TANAPA Dkt. Allan Kijazi kutoka kushoto kwake ni mwakilishi wa WMO akifuatiwa na mkurugenzi wa huduma za utabiri TMA Dkt. Hamza Kabelwa.




KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AAGIZA TAASISI ZINAZOMILIKI VITUO VYA HALI YA HEWA NCHINI KUSHIRIKIANA

Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wameandaa warsha ya siku moja ya wakuu wa taasisi zinazomiliki vituo vya hali ya hewa hapa nchini. Warsha hiyo ilifanyika katika hotel ya Kibo Palace mjini Arusha tarehe 30 April, 2015. Akifungua warsha hiyo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa kamati inayosimamia utekelezaji wa ‘Global Framework for Climate Services (GFCS)’ Dkt. Florence Turuka aliwaagiza wakuu hao wa taasis kushirikiana ili kuimarisha uwezo wa nchi katika kukusanya takwimu za hali ya hewa, kutoa tahadhari ya mapema ili kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.‘madhumuni ya warsha ni kujadiliana na kukubaliana namna bora ya kushirikiana juu ya ubadilishanaji wa taarifa na takwimu kutoka katika mitandao ya vituo vya hali ya hewa ili kutumia taarifa hizo ipasavyo katika shughuli mbali mbali za uchumi kwa ustawi wa jamii. Aidha, taarifa hizo zitasaidia katika kukabiliana na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa nchini ambayo ni muhimu kwa kuokoa maisha ya watu na mali zao.’ alizungumza Dkt. Turuka







Kwa upande wake Dkt. Agnes Kijazi, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni (WMO), aliwashukuru wakuu wa taasis zinazomiliki vituo vya hali ya hewa hapa nchini kwa kukubali kuhudhuria warsha hiyo. Dr. Kijazi aliongeza kwamba warsha hiyo ni muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa ‘WMO Integrated Global Observing System (WIGOS)’ hapa nchini. ‘Suala moja muhimu litakalojadiliwa katika warsha hii ni mkakati wa utekelezaji wa mpango wa WIGOS hapa nchini, mapendekezo yatakayotolewa katika warsha hii yatasaidia kutoa mwelekeo wa jinsi gani tutakavyotekeleza mpango wa WIGOS na Global Framework for climate services (GFCS) hapa nchini’ aliongeza Dkt Kijazi.




IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI OFISI YA UHUSIANO- TMA


No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...