Wednesday, May 20, 2015

WANANCHI WA UKANDA WA ZIWA NYASA KUNUFAIKA NA UPATIKANAJI WA TAARIFA MAALUM ZA HALI YA HEWA KWA WAVUVI, WAKULIMA, WAFUGAJI NA WASAFIRISHAJI KWA WAKATI.Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bi. Theo Ntara  ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela (watatu kutoka kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TMA Dkt. Hamza Kabelwa (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha inayohusu uboreshaji wa huduma za hali ya hewa katika maeneo ya Ziwa Nyasa kwa sekta ya wakulima na wafugaji, wavuvi na wasafirishaji, tarehe 14 Mei 2015  katika hotel ya Kyela Resort-Mbeya
Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani kupitia mpango wa utoaji wa huduma za hali ya hewa wa GFCS yaani “Global Framework for Climate Services” imezindua rasmi  huduma ya kutoa taarifa za hali ya hewa hususan tahadhari na utabiri mahususi kwa watumiaji wa ziwa nyasa. Taarifa hizo zitasamabazwa kupitia vyombo mali mbali vya habari ikiwemo redio za kijamii. Huduma hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Mei 2015 huko Kyela mkoani Mbeya na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dkt. Thea Ntara aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Katika kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu TMA wameandaa warsha ya “UBORESHAJI NA UAINISHAJI WA MAHITAJI YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA MAENEO YA ZIWA NYASA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI, WAVUVI NA WASAFIRISHAJI’’ iliyofanyika katika hotel ya Kyela Resort jijini Mbeya. Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bi. Thea Ntara alisema ‘Hivi karibuni tumeshuhudia matukio ya mvua ya mawe, mafuriko na radi katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya, hali hii imesababisha madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi. Nimatumaini yangu kuwa taarifa zinazopatikana kutoka kwa wananchi na wataalam mbalimbali kupitia semina hii zitaiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa kuboresha taarifa zake kwa umma na kuwawezesha watalaam kutoa ushauri stahiki unaozingatia taarifa za hali ya hewa’. Alizungumza hayo wakati akifungua rasmi warsha ya wadau wa hali ya hewa wanaotumia ziwa nyasa iliyowajumuisha wasafirishaji, wakulima, wavuvi, wafugaji, Ofisi ya Bandari, SUMATRA,usalama, Maafa, maliasili na vyombo vya habari.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi katika hotuba yake iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Utabiri TMA Dkt. Hamza Kabelwa alisema ‘Katika kuhakikisha TMA inazidi kuziboresha huduma zake, wataalam wa TMA wameweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela ili kupata uelewa zaidi wa majanga yanayoikumbuka wilaya hiyo na namna gani ya kuweza kufanyia kazi’.  ‘TMA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari imejikita katika kuhakikisha jamii inapata taarifa za hali ya hewa kwa wakati hususan kunapokuwa na vipindi vya matukio  ya hali mbaya ya hewa kama vile mvua kubwa, ukame, upepo mkali, mawimbi makubwa n.k  kwa lengo la kuisaidia jamii kuchukua tahadhari mapema ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na matukio hayo  hivyo kuchangia katika kuokoa maisha ya watu na mali zao’ alisema Dkt. Kijazi.

IMETOLEWA NA MONICA MUTONI AFISA HABARI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Tuesday, May 19, 2015

TMA SASA YAJIKITA KUOKOA MAISHA NA MALI ZA WATUMIAJI WA ZIWA NYASA KWA KUTOA HUDUMA MAALUM ZA HALI YA HEWA

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa akisoma hotuba ya Dkt. Agnes Kijazi katika ufunguzi wa uboreshaji wa huduma za hali za hali ya hewa ukanda wa Ziwa Nyasa uliyofanyika tarehe 11 Mei 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kyela Resort, Kyela-Mbeya.

Mgeni rasmi na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Dkt. Thea Ntara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela akihutubia hotuba ya Mhe. Abbas Kandoro wananchi walioshiriki katika ufunguzi wa uboreshaji wa huduma za hali za hali ya hewa ukanda wa Ziwa Nyasa uliyofanyika tarehe 11 Mei 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kyela Resort, Kyela-Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi TMA Dkt. Pascal Waniha akitoa neno la shukrani kwa niaba ya TMA kwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa uboreshaji wa huduma za hali za hali ya hewa ukanda wa Ziwa Nyasa uliyofanyika tarehe 11 Mei 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kyela Resort, Kyela-Mbeya.
Baadhi ya washiriki wa ufunguzi wa uboreshaji wa huduma za hali za hali ya hewa ukanda wa Ziwa Nyasa uliyofanyika tarehe 11 Mei 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kyela Resort, Kyela-Mbeya.


Mgeni rasmi akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari baada ya kufunga rasmi uboreshaji wa huduma za hali za hali ya hewa ukanda wa Ziwa Nyasa uliyofanyika tarehe 11 Mei 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kyela Resort, Kyela-Mbeya.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya ufunguzi wa uboreshaji wa huduma za hali za hali ya hewa ukanda wa Ziwa Nyasa uliyofanyika tarehe 11 Mei 2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kyela Resort, Kyela-Mbeya.

Monday, May 4, 2015

WARSHA YA WAKUU WA TAASISI ZINAZOMILIKI VITUO VYA HALI YA HEWA NCHINI YAFANYIKA MJINI ARUSHA

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, mkurugenzi wa Kitengio cha Maafa Brigedia Jenerali Mbazi Msuya ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha ya wakuu wa taasisi wanaomiliki vituo vya hali ya hewa nchini, iliyofanyika Arusha katika hoteli ya Kibo Palace tarehe 30 Aprili 2015.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania  (TMA)  Dkt. Agnes Kijazi na kushoto kwake ni mwakilishi kutoka Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Elijah Mukhala
Mwezeshaji Bw. Augustine Kanemba akimkaribisha mwakilishi kutoka WMO, Dkt. Elijah Mukhala kutoa nasaha zake katika warsha hiyo.
Mkurugenzi Mkuu TMA akitoa hotuba fupi wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuhutubia wanawarsha
Mgeni rasmi Brigedia jenerali Mbazi Msuya akihutubia wakuu wataasisi zinazomiliki vituo vya hali ya hewa wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya wanawarsha wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha waliokaa kutoka kulia kwa mgeni rasmi ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Kijazi, mkurugenzi kitengo cha usalama wa chakula, Kilimo Bw. Ombaeli Lemweli na mkurugenzi mkuu TANAPA Dkt. Allan Kijazi kutoka kushoto kwake ni mwakilishi wa WMO akifuatiwa na mkurugenzi wa huduma za utabiri TMA Dkt. Hamza Kabelwa.
KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AAGIZA TAASISI ZINAZOMILIKI VITUO VYA HALI YA HEWA NCHINI KUSHIRIKIANA

Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wameandaa warsha ya siku moja ya wakuu wa taasisi zinazomiliki vituo vya hali ya hewa hapa nchini. Warsha hiyo ilifanyika katika hotel ya Kibo Palace mjini Arusha tarehe 30 April, 2015. Akifungua warsha hiyo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa kamati inayosimamia utekelezaji wa ‘Global Framework for Climate Services (GFCS)’ Dkt. Florence Turuka aliwaagiza wakuu hao wa taasis kushirikiana ili kuimarisha uwezo wa nchi katika kukusanya takwimu za hali ya hewa, kutoa tahadhari ya mapema ili kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.‘madhumuni ya warsha ni kujadiliana na kukubaliana namna bora ya kushirikiana juu ya ubadilishanaji wa taarifa na takwimu kutoka katika mitandao ya vituo vya hali ya hewa ili kutumia taarifa hizo ipasavyo katika shughuli mbali mbali za uchumi kwa ustawi wa jamii. Aidha, taarifa hizo zitasaidia katika kukabiliana na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa nchini ambayo ni muhimu kwa kuokoa maisha ya watu na mali zao.’ alizungumza Dkt. TurukaKwa upande wake Dkt. Agnes Kijazi, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni (WMO), aliwashukuru wakuu wa taasis zinazomiliki vituo vya hali ya hewa hapa nchini kwa kukubali kuhudhuria warsha hiyo. Dr. Kijazi aliongeza kwamba warsha hiyo ni muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa ‘WMO Integrated Global Observing System (WIGOS)’ hapa nchini. ‘Suala moja muhimu litakalojadiliwa katika warsha hii ni mkakati wa utekelezaji wa mpango wa WIGOS hapa nchini, mapendekezo yatakayotolewa katika warsha hii yatasaidia kutoa mwelekeo wa jinsi gani tutakavyotekeleza mpango wa WIGOS na Global Framework for climate services (GFCS) hapa nchini’ aliongeza Dkt Kijazi.
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI OFISI YA UHUSIANO- TMA