Saturday, January 17, 2015

TMA YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA TEKNOLOJIA YA MFUMO WA KIDIGITAL WA UKUSANYAJI, UANDAAJI NA UTUMAJI WA TAARIFA ZA UANGAZI WA HALI YA HEWA (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) NA MFUMO WA USAMBAZAJI WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KWA USAFIRI WA ANGA (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu TMA Bw. Ibrahim Nassib akifungua warsha ya mafunzo ya utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa kidigital wa ukusanyaji, uandaaji na utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) na mfumo wa usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS), kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Dkt. Hamza Kabelwa

Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa kidigital wa ukusanyaji, uandaaji na utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) na mfumo wa usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS) kutoka katika vituo 28  vya Mamlaka ya Hali ya Hewa vya uangazi wa hali ya hewa vinavyo pima hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania


Madhumuni ya warsha hii ya mafunzo ni kujifunza kuongeza ubora wa uangazi wa hali ya hewa kwa njia za teknolojia ya kisasa kabisa. Aidha, mafunzo haya yanalenga katika maandalizi ya kuanza kutumika kwa teknolojia hii katika vituo vyote nchini.

Mifumo hii imetengenezwa na wataalamu wetu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Mifumo hiyo ni:

1. Mfumo wa kidigitali wa Ukusanyaji, Uandaaji na Utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (Digital Meteorological Observatory (DMO)) na

2. Mfumo wa Usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa Usafiri wa Anga (Meteorological Aviation Information System (MAIS)).


Mifumo hii itapunguza  gharama za uendeshaji zinazotokana  na utumiaji wa karatasi na kuweka kumbu kumbu, kuboresha mfumo wa mawasiliano ndani na nje ya nchi kwa maana ya ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kutokana na mahitaji na viwango vya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization).


Hali kadhalika, teknolojia hii inarahisisha ufuatiliaji wa utendaji kazi kwa watoa huduma na kuwawezesha wadau kutoa maoni ya huduma za hali ya hewa kwa urahisi na haraka zaidi kupitia mifumo hiyo.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...