Tuesday, January 20, 2015

WARSHA YA MFUMO WA KIMATAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA UWASILILISHWAJI WA RIPOTI YA IPCC KAMA ILIVYOJADILIWA KATIKA MKUTANO WA 20 (COP20) WA MABADILIKO YA HALI YA HEWAMgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu- TMA Dkt. Agnes Kijazi akipata utambulisho wa washiriki wa warsha ya Mfumo wa Kimataifa wa huduma za hali ya hewa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa Barani Afrika na uwasilishwaji wa ripoti ya IPCC kama ilivyojadiliwa katika mkutano wa 20 (COP20) wa mabadiliko ya hali ya hewa iliyofanyika, Kibaha. Tarehe 20 Januari 2015.

   
 Bi. Juwalia Mshana akiwa mmoja wa washiriki wa warsha ya Mfumo wa Kimataifa wa huduma za hali ya hewa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa Barani Afrika na uwasilishwaji wa ripoti ya IPCC kama ilivyojadiliwa katika mkutano wa 20 (COP20) wa mabadiliko ya hali ya hewa iliyofanyika, Kibaha. Tarehe 20 Januari 2015 akijitambulisha kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi  huduma za utafiti na matumizi-TMA Dkt. Ladislaus Chang'a akimkaribisha mgeni rasmi ili afungue warsha rasmi
Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu- TMA Dkt. Agnes Kijazi akifungua rasmi warsha ya mfumo wa Kimataifa wa huduma za hali ya hewa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa Barani Afrika na uwasilishwaji wa ripoti ya IPCC kama ilivyojadiliwa katika mkutano wa 20 (COP20) wa mabadiliko ya hali ya hewa iliyofanyika, Kibaha. Tarehe 20 Januari 2015.

Baadhi ya washiriki wa warsha ya mfumo wa Kimataifa wa huduma za hali ya hewa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa Barani Afrika na uwasilishwaji wa ripoti ya IPCC kama ilivyojadiliwa katika mkutano wa 20 (COP20) wa mabadiliko ya hali ya hewa iliyofanyika, Kibaha. Tarehe 20 Januari 2015.

Mmoja wa mshiriki kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Prof. Pius Yanda akifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi

Prof. Pius Yanda akiongoza mjadala wa warsha wakati wa kipindi cha majadiliano

Mkurugenzi Mkuu-TMA akishiriki katika majadiliano ya warsha
Meneja wa TMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Issa Hamad akichangia jambo katika warsha hiyo
Washiriki wa warsha  katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa warsha hiyo

Washiriki wa warsha hiyo ni kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais (VPO), vyuo vikuu (SUA na UDSM), Asasi za kiraia (PAKAYA), wakuu wa vituo vya hali ya hewa kanda zote Tanzania (Mwanza, Mbeya,Morogoro, Tabora, Dodoma,Mtwara na Zanzibar).Saturday, January 17, 2015

TMA YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA TEKNOLOJIA YA MFUMO WA KIDIGITAL WA UKUSANYAJI, UANDAAJI NA UTUMAJI WA TAARIFA ZA UANGAZI WA HALI YA HEWA (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) NA MFUMO WA USAMBAZAJI WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KWA USAFIRI WA ANGA (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu TMA Bw. Ibrahim Nassib akifungua warsha ya mafunzo ya utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa kidigital wa ukusanyaji, uandaaji na utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) na mfumo wa usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS), kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Dkt. Hamza Kabelwa

Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa kidigital wa ukusanyaji, uandaaji na utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) na mfumo wa usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS) kutoka katika vituo 28  vya Mamlaka ya Hali ya Hewa vya uangazi wa hali ya hewa vinavyo pima hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania


Madhumuni ya warsha hii ya mafunzo ni kujifunza kuongeza ubora wa uangazi wa hali ya hewa kwa njia za teknolojia ya kisasa kabisa. Aidha, mafunzo haya yanalenga katika maandalizi ya kuanza kutumika kwa teknolojia hii katika vituo vyote nchini.

Mifumo hii imetengenezwa na wataalamu wetu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Mifumo hiyo ni:

1. Mfumo wa kidigitali wa Ukusanyaji, Uandaaji na Utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (Digital Meteorological Observatory (DMO)) na

2. Mfumo wa Usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa Usafiri wa Anga (Meteorological Aviation Information System (MAIS)).


Mifumo hii itapunguza  gharama za uendeshaji zinazotokana  na utumiaji wa karatasi na kuweka kumbu kumbu, kuboresha mfumo wa mawasiliano ndani na nje ya nchi kwa maana ya ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kutokana na mahitaji na viwango vya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization).


Hali kadhalika, teknolojia hii inarahisisha ufuatiliaji wa utendaji kazi kwa watoa huduma na kuwawezesha wadau kutoa maoni ya huduma za hali ya hewa kwa urahisi na haraka zaidi kupitia mifumo hiyo.