Wednesday, December 31, 2014

MKURUGENZI MKUU TMA ATOA MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA JANUARI -FEBRUARI 2015

Mkurugenzi Mkuu wa TMA akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa utabiri wa mvua za Januari hadi Februari 2015
Wanahabari wakichukua habari kuhusiana na mwelekeo wa utabiri wa mvua za Januari hadi Februari 2015 katika ukumbi wa mikutano wa TMA
NB: Kupata taarifa ya kina kuhusiana na utabiri huo ingia www.meteo.go.tz


Sunday, December 21, 2014

BODI YA USHAURI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA CHINI YA UENYEKITI WA BW. MORISSON MLAKI YAFANYA UKAGUZI WA MIRADI MBALIMBALI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA JIJINI MWANZAMhandisi wa huduma za Radar Bw. Lemmy Mganga akitoa maelezo ya eneo la mradi kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TMA walipotembelea mradi huo mkoani Mwanza  katika milima ya Kiseke-Ilemela 
: Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA Bw. Morisson Mlaki akipata maelezo ya kina kutoka kwa mtaalam toka Ufaransa
Mhandisi wa huduma za Radar Bw. Lemmy Mganga akiendelea kutoa maelezo zaidi ya utendaji kazi wa radar ya hali ya hewa iliyopo Mwanza


Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA Bw. Morisson Mlaki pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi wakifanya mahojiano na wanahabari walioambatana na ujumbe huo

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA Bw. Morisson Mlaki akisisitiza jambo kwa wanahabari
Mhandisi wa huduma za Radar Bw. Lemmy Mganga akitoa ufafanuzi kwa wanahabari

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA Bw. Morisson Mlaki, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi, wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Menejiment ya TMA pamoja na wahandisi kutoka TMA na Ufaransa katika picha ya pamoja walipotembelea mradi wa Rada ya hali ya hewa, Mwanza


Mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya ushauri ya TMA wakipata maelezo ya uchambuzi wa taarifa za hali ya hewa kupitia radar katika ofisi za Hali ya Hewa zilizopo katika uwanja wa ndege wa Mwanza
Mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya ushauri ya TMA wakipata maelezo ya taarifa za hali ya hewa kwa matumizi ya ziwani zitolewazo na ofisi za Hali ya Hewa zilizopo katika Bandari ya Mwanza kutoka kwa meneja wa Kanda ya Ziwa Bw. Michael Likunama