Thursday, June 26, 2014

MKURUGENZI MKUU TMA ASHIRIKI MKUTANO WA 66 WA KAMATI KUU YA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WMO-EC).


Rais wa Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Prof. David Grimes  ( wanne kushoto kutoka mstari wa mbele) na Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Michel Jarraud (watatu kutoka kushoto mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO EC). Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt Agnes Kijazi (wa kwanza kutoka kushoto waliosimama) akiwa miongoni mwa wajumbe 37 wa kamati hiyo kuu ya WMO. 



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati  kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani anashiriki mkutano wa 66 wa Kamati Kuu ulioanza tarehe 18 Juni 2014 huko Geneva. Mkutano wa mwaka huu utajadili masuala ya hali ya hewa katika maeneo yafuatayo : Upunguzaji wa madhara yatokanayo na hali mbaya ya hewa, Utoaji huduma za hali ya hewa, mpango maalum wa kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinawafikia walengwa zikiwa na ubora (Global Framework for Climate Services-GFCS), Mkakati endelevu  wa kujenga uwezo, mfumo wa uangazi wa hali ya hewa wa Shirika la Hali ya Hewa Dunia na shughuli za utafiti. Kwa maelezo zaidi tembelea www.wmo.int   
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI , AFISA UHUSIANO,TMA

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...